IQNA

Mafundisho ya Uislamu yanadhamini misingi imara ya familia

12:47 - December 11, 2008
Habari ID: 1717960
Sheria na mafundisho ya Uislamu yanamfikisha mwanadamu katika ukamilifu na si katika kushibisha tu mahitaji yake, tofauti na mifumo ya kifikra ya Magharibi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu Ayatullah Muhammad Ali Tas’khiri katika kongamano lililochunguza sheria zinazohusu masuala ya familia na afya ya uzazi katika mtazamo wa Kiislamu. Ayatullah Tas’khiri amesema: Mfumo wa familia unapewa umuhimu mkubwa katika Uislamu na sehemu kubwa ya sheria za dini hiyo katika masuala yote ya maisha imejengeka juu ya msingi wa familia kama vile mirathi, maisha ya unyumba na kadhalika.
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa afya ya uzazi, malezi ya watoto, kuchunga misingi ya maadili mema na afya katika masuala ya maingiliano ya kujamiiana kwa ajili ya kufikia ukamilifu wa kibinadamu na mahusiano salama ya kujamiiana ni miongoni mwa masuala yaliyopewa umuhimu katika sheria za Kiislamu. Amesema kuwa nchi za Magharibi zinasisitiza tu juu ya afya ya kutunga mimba kwa lengo la kueneza uchupaji mipaka katika maingiliano ya ngono na si kwa shabaha ya kuimarisha misingi ya familia.
Ayatullah Tas’khiri ameashiria pia mchango wa dini katika utamaduni wa jamii na akasema: Njia ya utatuzi wa masuala na matatizo ya familia inaweza kupatikana katika mafundisho ya Kiislamu.
Kongamano la Uchunguzi wa Sheria za Masuala ya Familia na Afya ya Uzazi Katika Mtazamo wa Kiislamu” limesimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu na kuhudhuriwa na Waziri wa Afya wa Iran, mwakilishi wa Shirika la Jamii la Umoja wa Mataifa nchini Iran, wahadhiri wa vyuo vikuu na wageni waalikwa kutoka nje ya nchi. 332214

captcha