IQNA

Umoja wa Waislamu wa Iraq kujadiliwa katika mkutano wa Baghdad

11:32 - December 13, 2008
Habari ID: 1718425
Mkutano wa Umoja kati ya Waislamu wa Iraq unatazamiwa kufanyika hivi karibuni mjini Baghdad.
Mkutano huo unafanyika kwa shabaha ya kujenga umoja na mshikamano zaidi kati ya Waislamu wa nchi hiyo iliyovamiwa na Marekani na waitifaki wake.
Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa kidini na kisiasa wa madhehebu ya Shia na Suni ambao watahuisha mtakaba wa Makka.
Mkataba wa Makka ulitolewa mwaka 2006 katika kongamano la kimataifa lililofanyika kwenye mji mtakatifu wa Makka kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu wa Kishia na Kisuni wa Iraq. 332484

captcha