Afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje wa utawala ghasibu wa Israel amethibitisha habari hiyo na kudai kuwa Richard Falk anaunga mkono harakati za kigaidi za chama cha Hamas na kwamba amefananisha mwenendo wa Israel dhidi ya Wapalestina na jinai zilizofanywa na Manazi wa Ujerumani dhidi ya Mayahudi.
Mkaguzi maalumu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Richard Falk alisema jana kwamba siasa za Israel dhidi ya Wapalestina ni jinai dhidi ya binadamu, suala ambalo limewakasirisha mno viongozi wa utawala huo ghasibu.
Falk aliteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza hali ya haki za binadamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 334901