Ripoti ya Newsweek imesema: Nasrullah anapendwa mno na wananchi katika nchi za Kiarabu kwa sababu ya kuushinda utawala ghasibu wa Israel katika vita vya siku 33 mwaka 2006.
Jarida hilo limeandika kuwa wapiganaji wa Hizbullah walilidhalilisha jeshi la Israel katika vita siku 33 huko Lebanon na Sayyid Hassan Nasrullah anatambuliwa kuwa shujaa katika ulimwengu wa Kiarabu.
Jarida la Newsweek ambalo hutoa orodha ya majina ya watu wenye ushawishi mkubwa kila mwaka, limeorodhesha majina ya watu hamsini kama shakhsia wenye ushawishi mkubwa duniani akiwemo Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ambaye limesema: Amepata ushawishi kutokana na nchi yake kuwa na akiba kubwa ya mafuta na taathira zake kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa!
338106