Viongozi wa Kiislamu nchini Lebanon wametoa taarifa wakilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutuma vikosi vya kimatiafa kwa lengo la kuuzuia utawala haramu wa Israel kutekeleza jinai zaidi dhidi Wapalestina wanaodhulumiwa huko Gaza. Aidha wamesema, vikosi hivyo vya kimatiafa vinapaswa kuwapa himaya Wagaza na kuvunja mzingiro wa Kizayuni katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Mustaqbal linalochapishwa Beirut, viongozi wa Kiislamu nchini Lebanon wamekutana katika taasisi ya Darul Ifta kutathmini jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza. Maulamaa hao wa Kiislamu wametoa wito kwa Wapalestina kudumisha umoja. Wamesema kuna umuhimu kwa Wapalestina wote kuweka kando hitilafu zao ili waweze kukabiliana na adui ghasibu na Mzayuni. Viongozi hao wa Kiislamu aidha wamewataka Walebanon kufanya maandamano zaidi kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa na pia kudumisha umoja ili Lebanon isishambuliwe tena na Israel.
Kikao hicho kilidhuhuriwa na Mufti wa Lebanon Sheikh Muhammad Rashid Qabani, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon Sheikh Abdul Amir Qublani na Sheikh Naim Hassan, kiongozi wa jamii ya Wadruzi nchini humo. 340235