IQNA

Ni lazima Wazayuni wahisi kwamba Waislamu wanawaunga mkono Wapalestina

10:51 - January 01, 2009
Habari ID: 1725886
Katika mazungumzo yake ya simu na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Saudi Arabia, Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Wazayuni wanaotekeleza jinai dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza wanapaswa kulazimishwa kukubali kwamba Waislamu wote wanawaunga mkono Wapalestina hao, la sivyo, wataendelea kutekeleza na hata kuzidisha jinai hizo dhidi ya wananchi hao madhlumu.
Katika mazungumzo hayo na Swaleh bin Abdallah bin Hamid, Larijani amebainisha masikitiko yake makubwa kuhusiana na hali ya kutisha ya Wapalestina wakazi wa Gaza na kusisitiza kwamba, marafiki halisi wa Wapalestina wamesikitishwa sana na masaibu yanayowapata wananchi wa Palestina. Amesema, matuko yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza si jambo jingine isipokuwa mauaji na jinai zinazotekelezwa na Wazayuni dhidi ya binadamu. Amesema, kwa kushambulia mahospitali, misikiti na makazi ya raia, utawala ghasibu wa Israel imekanyaga misingi yote ya kibinadamu na sheria za kimataifa. Amesema matukio hayo ya kusikitisha yanayoendelea kutekelezwa katika Ukanda wa Gaza yanaziwajibisha nchi zote za Kiislamu kutekeleza majukumu yao ya kidini na kiutu ya kuwatetea na kuwalinda wananchi wasio na ulinzi wa ukanda huo dhidi ya hujuma ya kinyama ya Wazayuni. Amesema, utawala huo haramu unapasa kufanywa kuamini kwamba Waislamu wote ni kitu kimoja na wanaowaunga mkono wenzao wa Palestina la sivyo utazidisha jinai zake za kinyama dhidi ya Wapalestina hao wasio na ulinzi. Amesema kuna udharura mkubwa wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu kufanya kikao cha dharura ili kuchunguza na kusimamisha mara moja mauaji ya umati yanayotekelezwa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina. Katika mazungumzo hayo, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Saudi Arabia pia amesema kuwa ni jukumu la Waislamu wote kuwatetea wananchi wa Palestina dhidi ya mashambulio ya kinyama ya Wazayuni. 341518
captcha