IQNA

Maaskofu wa makanisa ya Quds watoa wito wa kukomeshwa mauaji ya Israel huko Gaza

11:54 - January 01, 2009
Habari ID: 1725916
Maaskofu wa makanisa ya mji wa Quds Tukufu wametoa taarifa wakiutaka utawala ghasibu wa Israel kukomesha mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo ya viongozi wa Kikristo wa Palestina akiwemo Askofu Theophilos III wa kanisa la Orthodox na Maaskofu Fouad Twal na Torkom II wa kanisa la Kiarmenia, wametoa pendekezo la kutangazwa tarehe 4 Januari kuwa ni siku ya 'Uadilifu na Amani' katika ardhi za Palestina.
Maaskofu hao wa Kikristo wamelaani mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika eneo la Gaza na kusisitiza kwamba, wana wasiwasi mkubwa kuhusu mauaji yanayofanyika dhidi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina katika ukanda huo. Vilevile wamelaani vitendo vya utumiaji mabavu duniani kote na wameitaka Israel kukomesha mauaji ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Maaskofu wa makanisa ya Quds wameitaka jamii ya kimataifa kutekeleza majukumu yake kuhusu Palestina, kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Gaza na kusitisha umwagaji damu unaofanyika katika eneo hilo.
Maaskofu hao pia wameyausia makundi ya Kipalestina kutupilia mbali hitilafu zao za ndani na kufanya mambo yenye maslahi kwa wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. 341680

captcha