IQNA

UNRWA yatahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea maafa katika Ukanda wa Gaza

11:24 - January 15, 2009
Habari ID: 1731290
Shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko wa ugonjwa wa waba katika Ukanda wa Gaza.
John Ging Mkurugenzi wa operesheni za Unrwa ametahadharisha juu ya hali mbaya ya kiafya ukiwemo mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na maradhi mengineyo kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa, zaidi ya Wapalestina laki tano wakaazi wa Gaza, khususan wa maeneo ya katikati mwa ukanda huo hawana maji safi kwa zaidi ya wiki moja sasa.
John Ging amesema, kiwango cha uzalishaji wa umeme huko Gaza kimepungua kutokana na uhaba wa mafuta na kwamba hivi sasa kiwanda za kuzalisha nguvu za umeme kinazalisha asilimia nne tu ya umeme, ambao hutumika pia mahospitalini.
Hii ni katika hali ambayo, Mundhar Shiblaq Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Maji wa
vitongoji vilivyoko katika pwani ya Ukanda wa Gaza amesema kuwa, raia wa eneo hilo hawana maji safi na salama kufuatia kuendelea kwa mashambulizi ya jeshi la Israel katika eneo hilo.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeharibu miundombinu na taasiswi muhimu za kijamii katika Ukanda wa Gaza na umekuwa ukizuia misaada ya kibinadamu iliyopelekwa kwa raia wa eneo hilo. 348193

captcha