IQNA

Taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa Wapalestina zinaitia kiwewe Israel

9:34 - January 20, 2009
Habari ID: 1733310
Israel imeingiwa kiwewe na wahaka kutokana na taathira za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ambayo yalifanyika kwa msingi wa kupambana na dhulma kwa taifa la Palestina na serikali halali ya Hamas.
Hayo yamesemwa na Amin Sahili ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kisiasa na kuongeza kuwa: Kuenea kwa fikra za Mapinduzi ya Kiislamu na miongozo ya hayati Imam Khomeini ya kupambana na dhulma na madhalimu ambayo inawafunza Waislamu kupambana na maadui kwa kutumia silaha ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, kunapingana na siasa za kutumia mabavu za Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu zinazouogopa utawala huo haramu.
Sahili amesema kuwa maroketi ya Hamas yameonyesha taswira ya mapambano ya taifa la Palestina na kusisitiza kwamba, Israel inapinga aina yoyote ya kusimama kidete na mapambano ya wananchi wa Palestina na mataifa mengine. Amesema kuwa wananchi wa Gaza wanapambana na jeshi la utawala unaokalia kwa mabavu ardhi na nchi yao na wakati huo huo wananyimwa haki ya kukabiliana na utawala huo dhalimu, kwani wanapoamua kupambana wanashutumiwa kuwa ni magaidi na watenda jinai.
Mtaalamu huo wa masuala ya kisiasa amesema kuwa, mwenendo wa serikali ya Misri kuhusiana na kadhia ya Palestina si wa kibinadamu na unakatisha tamaa. Amesisitiza kuwa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu hazitaki kuiona Hamas ikiwa harakati ya mapambano na zinahimiza kuwa harakati hiyo inapaswa kujishughulisha tu na masuala ya kisiasa. 349619

captcha