IQNA

Le Monde lakiri, vyombo vya habari vya Israel vimeficha Holocaust ya Gaza

10:48 - January 21, 2009
Habari ID: 1733941
Gazeti la Le Monde la Ufaransa limechapisha makala iliyopewa anwani ya "Nusu ya Ukweli" likisema kuwa: Vyombo vya habari vya Israel vilipasha habari za nusu ya ukweli wa mambo kuhusu jinai za utawala huo katika vita vya siku 22 kwenye Ukanda wa Gaza.
Makala hiyo imesema kuwa kanali ya pili televisheni ya Israel iliyotengwa kwa ajili ya kuripoti habari za mashambulizi ya kijeshi ya Israel ilikuwa ikipasha habari kwa masaa 10 tu kwa siku na habari zake nyingi kuhusu mauaji ya wakazi wa Gaza zilikuwa zikichujwa.
Gazeti la Ufaransa la Le Monde limemnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani wa kanali ya pili ya televisheni ya Israel Arad Nir akikiri kwamba kanali hiyo ilieleza nusu ya ukweli wa mambo kuhusu vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza kwani kimsingi watu wa Israel hawafahamu chocote.
Makala ya gazeti la Le Monde imemalizia kwa kuandika kwamba: Vita vya Gaza vimeimarisha zaidi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas na kwamba matokeo ya vita hivyo ni kudhoofika kwa nafasi ya Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas huko katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan. 351598


captcha