Suzan Winter, mbunge wa chama cha mrengo wa kulia chenye misimamo mikali cha FPO nchini Austria amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela na kulipa faini ya Euro elfu 24 kwa kupatikana na hatia ya kutoa matamshi yanayoubera Uislamu na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limeripoti kuwa, Suzan Winter, mwakilishi wa mji wa Graz katika bunge la Austria Januari 2008 aliutusi Uislamu kuwa ni dini ya kutumia mabavu na akamvunjia heshima Mtume Muhammad (saw), jambo ambalo lilizusha wasiwasi na malalamiko ya wananchi wa Austria hususan Rais Heinz Fischer wa nchi hiyo.
Jamii ya Kiislamu ya Austria iliwasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya mbunge huyo kutokana na kutoa matamshi yanayobera itikadi za Uislamu na kufanya propaganda chafu dhidi ya dini hiyo. 352693