Hayo yamesemwa na Mahdi Sarami Mwanachama wa Baraza la Sera la Maonyesho ya Kwanza ya Kitaifa ya Vyombo ya Habari vya Dijitali nchini Iran. Akizungmza katika mji Mtakatifu wa Mash'had katika kongamano la 'Nafasi ya Vyombo Habari vya Dijitali katika Kuwapa Himaya Watu wa Gaza', amesema kuwa: "Vyombo vya habari vya dijitali vimeakisi ipasavyo matukio ya Gaza bila kubana chochote".
Amesema, vyombo vya habari vya dijitali husambaza habari kupitia intaneti, michezo ya kompyuta, simu za mkononi n.k. Amesema kuwa habari za dijitali huwafikia watu wengi na kwa kasi katika kipindi kifupi.
Sarami amesema, kuna haja ya kuimarisha mapambano ya Kiislamu kupitia njia za dijitali na ametoa wito kwa taasisi za Kiislamu kufanya hima kuimarisha uwezo wao katika sekta hiyo muhimu. 352795