IQNA

Ukurasa wa intaneti wa Mtume Muhammad (saw) kwa lugha kumi kuzinduliwa

12:10 - January 29, 2009
Habari ID: 1737416
Washiriki katika mkutano wa Kituo cha Kimataifa cha Kumuarifisha Mtume wa Uislamu wametoa wito wa kufunguliwa kituo cha intaneti cha kumuarifisha Mtume Muhammad (saw) kwa lugha kumi hai duniani.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu Abdullah bin Muhsin al Turki ambaye pia ndiye msimamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Kumuarifisha Mtume wa Uislamu, amesema kwamba suala litakalopewa kipaumbele zaidi na kituo hicho ni kumuarifisha Mtume Muhammad (saw) katika upeo wa kieneo na kimataifa na kwa lugha mbalimbali. Amesema, mfuko wa fedha za kudhamini utekelezaji wa mpango huo utaanzishwa hivi karibuni.
Al Turki amesema kuwa kituo hicho kitaanza kumuarifisha Mtume (saw) kwa lugha kumi hai za dunia na kwamba mipango ya kutumia lugha nyingine itafanyika hapo baadaye. Amesisitzia kuwa kazi hiyo itatekelezwa kwa kutumia uchapishaji wa vitabu, kanda, vipindi vya televisheni na kadhalika. Amesema kuwa mpango huo utaanza kwa kumuarifisha Mtume kwa wasiokuwa Waislamu kwa kutumia lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiurdu, Kituruki, Kibengali, Kiindonesia, Kichina na Kihindi.
Viongozi wa nchi za Kiislamu waliokutana hivi karibuni nchini Senegal walisisitiza juu ya ydharura wa kuanzishwa kituo cha kumtetea Mtume Muhammad (saw).
Malengo ya kituo hicho ni kumtambulisha Mtume wa Uislamu kwa wasio Waislamu, kusahihisha fikra zisizokuwa sahihi kuhusu Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu na kufafanua suna, sira na tabia zake njema katika kutatua matatizo ya wanadamu.
Ofisi kuu ya kituo hicho iko Riyadh, Saudi Arabia na itakuwa na matawi katika nchi mbalimbali. 824578
captcha