IQNA

Kuundwa kamati ya kisheria ya kuwafuatilia viongozi wa Israel

9:41 - February 04, 2009
Habari ID: 1739992
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu Ja’far Abdulsalam amesema kuwa imeundwa kamati ya kisheria ya kuwafuatilia na kuwafikisha viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mahakama ya kimataifa kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza.
Ja’far Abdulsalam amesema, kamati hiyo inajumuisha wanasheria na wataalamu wa sheria za kimataifa. Amesema kamati hiyo itakusanya ushahidi wa jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza na kuzikabidhi kwa mahakama ya kimataifa.
Ja’far Abdulsalam ambaye alikuwa akizungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa mkutano wa kimataifa uliochunguza jinai za vita vya Israel dhidi ya Gaza, amesema kuwa hujuma ya kinyama ya utawala huo wa Kizayuni imeharibi miundombinu ya eneo hilo kwa kadiri kwamba jumuiya za kimataifa na vyombo vya habari vimekadiria hasara iliyosababishwa na mashambulizi hayo kuwa ni karibu dola bilioni tatu.
Amesema kuwa washiriki katika mkutano huo wametoa wito wa kuanzishwa kanali ya televisheni ya satalaiti ya Kiislamu kwa lugha mbalimbali kwa shabaha ya kuwafahamisha watu wa Magharibi masaibu na mashaka yanayowasibu watu wa Palestina na mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia.
Amesema, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kitengo cha Habari cha Chuo Kikuu cha al Azhar Bakr Zaky Ibrahim akishirikiana na wataalamu wa fiqhi na wanafikra wa Kiislamu, watatayarisha utafiti linganishi na wa kielimu kuhusu faradhi ya jihadi katika dini ya Kiislamu na dini iliyopotoshwa ya Kiyahudi na kuwaelimisha Waislamu na walimwengu kuhusu itikadi zilizopotoshwa za Mayahudi katika uwanja wa mauaji ya wanawake na watoto wadogo wasiokuwa na hatia. 358766
captcha