Hayo yamesemwa na Muhammad Swadiq Kushki, mwanachama wa jopo la wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Khojah Nassir ad-Deen cha nchini Iran. Msomi huyo amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni tukio muhimu zaidi la karne ya 20 na kuongeza kuwa, ushindi wa mapinduzi hayo ulisambaratisha uwiyano na mahesabu ya watu wengi duniani.
Amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalileta mabadiliko makubwa katika pembe mbalimbali za dunia na kwamba, katika zama ambazo madola makubwa ya Magharibi yalikuwa yakihubiri kutenganishwa dini na siasa na kuwa serikali zisizozingatia dini ndizo zinazofaa kuendesha maisha ya mwandamu duniani, ghafla Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliibuka na kubatilisha kabisa propaganda hizo zisizo na msingi.
Swadiq Kushki amesisitiza kwamba, maendeleo mengi na makubwa ambayo Jamhuri ya Kiislamu imeyaleta katika kipindi hiki kifupi cha miongo mitatu, ni ishara na uthibitisho wa wazi kwamba serikali iliyosimama juu ya misingi ya dini ndiyo serikali bora zaidi inayomdhaminia mwanadamu saada ya dunia na huko Akhera.
Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amesema, Mapinduzi ya Kiislamu yameweza kutegemea mafundisho ya dini ya Kiislamu na busara ya viongozi wake, na hasa Imam Khomeini (MA) na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kuwasilisha fikra tofauti kabisa na ya Wamagharibi na kuthibitisha kiviendo kuwa ndiyo fikra bora zaidi inayoweza kumuongoza mwanadamu na kumdhaminia mahitaji yake yote hapa duaniani na kesho huko Akhera.
Amesema, kama alivyotabiri Imam Khomeini mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, mapinduzi haya yameweza kueneza kwa kiwango kikubwa mafundisho na mwamko wa Kiislamu katika pembe mbalimbali za dunia na hasa za Marekani na Ulaya, na hivyo kuwafanya Waislamu katika nchi hizo wapiganie haki zao ambazo zilikuwa zimeporwa na madola hayo ya kidhalimu. 360574