IQNA

Kiko cha 'uchunguzi wa mlingano wa sheria za familia katika nchi za Kiislamu' chaanza

10:17 - February 08, 2009
Habari ID: 1741459
Kikao cha kwanza cha kimataifa cha kunchunguza kimlingano sheria za familia katika nchi za Kiislamu kimeanza katika ukumbi wa Wizara ya Jihadi ya kilimo nchini Iran.
Kikao hicho ambacho kinahudhuriwa na wawakilishi wengi wa nchi za Kiislamu kinajaribu kuchunguza njia za kukurubisha pamoja fikra za nchi za Kiislamu kuhusiana na haki za familia, ushirikiano zaidi kuhusiana na masuala ya sheria za famiilia, njia za kuimarisha misingi ya familia na kunufaika na uzoefu wa nchi za Kiislamu kuhusiana na suala zima la haki za familia.
Hujjatul Islam wal Muslimeen Ali Akbar Rashad, mwanachama wa Baraza kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiutamaduni na Kifikra na vilevile Zahra Tabibzadeh Nuri, Mshauri wa Rais na Mkuu wa Taasisi ya Masuala ya Wanawake na Familia iliyo chini ya Ofisi ya Rais wa Iran ni miongoni mwa watu ambao wamehutubia kikao hicho.
Kikao hicho kitaendelea kwa muda wa siku tatu. 360466
captcha