Kwa mujibu wa mwandishi wetu mjini Beirut, Jumuiya ya Maulamaa wa Beirut imetoa taarifa na kumpongeza Mufti wa Misri Sheikh Ali Juma kwa sababu ya msimamo wake wa hivi karibuni ambapo aliwataka Waislamu kote duniani kuungana na kujiepusha na mifarakano na chuki.
Katika taarifa yao, maulamaa wa Lebanon wamesema: “Lengo letu katika Jumuiya ya Maulamaa wa Beirut inakupongeza kwa msimamo wako huu. Mwito wako kwa Umma ni jambo lonaloashiria ukweli kuwa sisi sote ni umma mmoja na hakuna tofauti kati ya Shia na Sunni. Sote tunalengwa na maadui wa umma wa Kiislamu ambao wanataka kutuhujumu. Umma wa Kiislamu sasa unahitaji umoja na mshikamano zaidi na kuwa na uangalifu mbele ya hatari zinazoutishia umma huu.
Hivi karibuni Mufti wa Misri Sheikh Ali Juma alitoa taarifa na kuwataka Waislamu kuhifadhi umoja wa neno na kujiepusha na mifarakano na chuki. Aidha waliwataka kujiepusha na kuzusha mifarakano kwani madola ya kibeberu daima yanakusudia kuzusha migongano baina ya Waisalmu. 361319