Kongamano hilo linahudhuriwa na wataalamu wa sheria za familia kutoka nchi mbalimbali duniani.
Wataalamu wa kitaifa na kimataifa katika kongamano hilo wamewasilisha makala kuhusu masuala kama vile; ‘uadilifu wa mwanamume na mwanamuke katika Uislamu’, ‘familia na uwezo wa kisheria’, ‘dhamana ya utekelezwaji sheria katika haki za familia katika Uislamu’, ‘kuteswa watoto katika familia’, ‘Watoto wanaolelewa vibaya’ na
‘haki ya mtoto katika nchi za Kiislamu’. 361218