Hitima hiyo ambayo pia kimefanyika kwa ajili ya kufungamana na akina mama wa Gaza ilifanyika kwa kusimama katika ufukwe wa Ramlat Al Baidhaa na wakati wa magharibi majina ya watoto mashahidi yalisomwa.
Mina Khalidi mmoja kati ya waandalizi wa hitima hiyo amesema kuwa: 'Baada ya kumalizika vita vya Gaza tulioana watu katika maeneo mengine ya dunia wamerejea katika maisha yao ya kawaida katika hali ambayo maisha ya watu wa Gaza hayajarejea katika hali ya kawaida hata kidogo. Watu wa Gaza wanaishi katika umasikini na ukimbizi na inaelekea hali hiyo imesahaulika".
Bi. Khalidi amesema, vita vimemalizika lakini umasikini na masaibu hayajamalizika na kwa hivyo walimwengu hawapaswi kusahau matatizo ya watu wa Gaza. Ameongeza kuwa hitima hiyo imefanyika sambamba katika nchi kadhaa duniani kama vile Ireland, Jordan, Libya, Umoja wa Falme za Kiarabu na Canada.
Bi.Khalidi amesema kuwa hitima ya mtoto wa kwanza kuuawa shahidi mikononi mwa makatili wa Kiisraeli imeanza kwa wito wa kususiwa bidhaa zinazotengenezwa katika viwanda vinavyofungamana na utawala wa Kizayuni kama Johnson & Johnson, Motorola, Coca-Cola na McDonald n.k. 362129