IQNA

Wafanyaziara wamiminika katika ziara la Abdul Adhim (as) sambamba na kuwadia mwezi wa Rabiul Awwal

10:50 - March 02, 2009
Habari ID: 1750217
Sambamba na kuwadia mwezi wa Rabiul Awwal wafanyaziara na watu wanaoishi karibu na ziara la Abdul Adhim Hassani (as) wamekuwa wakimiminika katika ziara hilo kwa lengo la kuukaribisha kwa shangwe mwezi huu mtukufu ambamo alizaliwa Mtume wetu Mtukufu Muhammad (saw).
Ripoti zinasema kuwa waumini wamekuwa wakimiminika katika ziara hilo kwa lengo la kuuaga mwezi wa Safar ambao unatajwa kuwa ni mwezi wa huzuni kutokana na kuaga dunia ndani yake kwa watukufu wa Nyumba ya Mtume (saw) akiwemo Mtume mwenyewe, na kuukaribisha mwezi wa Rabiul Awwal ambamo Mtume alizaliwa, na kumuomba Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwa Imam wa Zama (af).
Mwezi huu pia ni muhimu mno kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia ambapo tukio muhimu la Lailatul Mabit lilitokea. Tukio hilo linahusiana na hijra ya Mtume kutoka Makka kuelekea Madina ambapo alimwacha Imam Ali bin Abi Twalib (as) akiwa amelala kitandani kwake ili kuepuka njama ya makafiri wa Makka waliotaka kumuua.
Mwezi huu pia unahusiana na siku ya kuzaliwa Imam Ja'ffar Swadiq (as), ndoa ya Mtume (saw) na Bibi Khadija na kuanza kwa kipindi cha uimamu wa Imam Mahdi (af). 370813
captcha