Ofisi ya Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani katika jimbo la Minnesota imetangaza kuwa muswada huo unakiuka haki za wafuasi wa dini mbalimbali zinazotumia nembo za kidini.
Muswada huo ambao inasemekana umependekezwa kwa shabaha ya kuimarisha usalama wa taifa, unasisitiza kwamba watu pekee wanaoruhusiwa kuweka picha zenye vazi la hijabu katika leseni za kundeshea magari ni wale wanaolazimika kufanya hivyo kwa sababu za kitiba.
Sheria za sasa za Marekani zinaruhusu kuwa na picha zenye vazi la hijabu katika pasi za kusafiria na vitambulisho mbalimbali.
Siku kadhaa zilizopita uliwasilishwa muswada kama huo huko Oklahoma lakini haukupasishwa kutokana na juhudi za Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani. 373144