IQNA

Mbunge wa Kyrgyzistan apinga marufuku ya vazi la hijabu

14:41 - March 07, 2009
Habari ID: 1752792
Mwakilishi wa Bunge la Kyrgyzistan ametangaza upinzani wake dhidi ya marufuku ya vazi la hijabu katika taasisi za elimu nchini humo.
Ali Shir Sabirov amesema kuwa hakubaliani na uamuzi wa Wizara ya Elimu ya Kyrgyzistan wa kupiga marufuku vazi la hijabu ya Kiislamu.
Amesema kuwa uamuzi wa wizara hiyo hauoani na vipengee vya katiba ya Kyrgyzistan na kwamba amewasilisha rasmi upinzani wake kimaandishi katika Wizara ya Elimu ya nchi hiyo.
Wizara ya Elimu ya Kyrgyzistan imepiga marufuku vazi la hijabu ya Kiislamu katika taasisi za elimu. Mbunge Ali Shir Sabirov ameutaja uamuzi huo kuwa si wa kiadilifu na kwamba hauna msingi wa kisheria. 373547

captcha