Sheikh Hussein Hafidhov amesema kuwa uamuzi huo unakiuka haki za wanawake wa Kiislamu wa Bulgaria na kuwawekea vizuizi na mipaka.
Serikali ya Bulgaria Alkhamisi iliyopita iliwasilisha muswada bungeni unautaka kupigwa marufuku vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu na nembo za kidini katika skuli za nchi hiyo.
Muswada huo unapaswa kupasishwa na Bunge kabla ya kuanza kutekelezwa.
Bulgaria ambayo ina jamii ya Waislamu milioni 12 ni mwanachama pekee wa Umoja wa Ulaya ambaye Waislamu wake wengi ni wenyeji wa nchi hiyo.
Kabla ya Bulgaria, Ufaransa na nchi nyingine kadhaa za Ulaya zimepiga marufuku vazi la hijabu katika shule na idara za serikali.
Waislamu daima wamekuwa wakisisitiza kuwa vazi la hijabu si nembo ya kidini bali ni wajibu unaopaswa kutekelezwa na wanawake wote wa Kiislamu. 380729