IQNA

Iran kusimamisha uhusiano wa kiuchumi na waungaji mkono wa ugaidi

11:18 - April 05, 2009
Habari ID: 1760378
Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wiki hii linatazamiwa kuchunguza rasimu iliyowasilishwa na Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje kuhusu udharura wa kutazamwa upya uhusiano wa kibiashara na kiuchumi wa Tehran na nchi zinazounga mkono ugaidi.
Rasimu hiyo itaanza kujadiliwa wakati wabunge watakaporejea kazini baada ya kukamilisha likizo za mwaka mpya wa Hijria Shamsia na sikukuu ya Nairuzi.
Mijadala ya kuchunguza rasimu ya kutazamwa upya uhusiano wa kiuchumi wa Iran na nchi zinazounga mkono ugaidi itafanyika katika siku za Jumapili ya leo, Jumanne na Jumatano ijayo. 382494

captcha