Kituo hicho cha utafiti cha Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimesema kuwa hakuna tatizo lolote la kisheria la kujiunga Iran na kituo kilichotajwa cha utafiti wa kiuchumi, kijamii na kitakwimu kwa sababu kinahesabiwa kuwa moja ya taasisi na idara muhimu za Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC ambapo Iran tayari ni mwanachama muhimu na hai.
Kituo hicho cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran au kwa ibara nyingine Bunge, kimesema kuwa Iran inapasa kulipa ada yake ya uanachama kwa wakati na wakati huohuo kujihusisha zaidi na utafiti pamoja na uendeshaji wa kituo hicho ili kunufaika kwa kila njia na huduma za kituo hicho.
Kimesisitiza kwamba, Iran inapasa kuimarisha nafasi yake katika kituo hicho cha utafiti cha nchi za Kiislamu ili kustawisha ushirikiano wa kieneo na kimataifa kwa maslahi ya umma wa Kiislamu. 382285