Huku akishiria kutajwa mwaka huu wa 1388 wa Kiirani na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni mwaka wa kurekebisha mwenendo wa matumizi, Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu amesema kuwa utamaduni na sanaa ya Iran imejiandaa kutekeleza nara hiyo muhimu.
Akizungumzia suala hilo katika hadhara ya wafanyakazi wa wizara hiyo, Waziri Muhammad Hussein Safarharandi amesema kuwa duru mbalimbali za kiutamaduni nchini yakiwemo magazeti, filamu na vitabu vinapasa kufanya juhudi za kutekeleza kivitendo ujumbe huo muhimu wa Kiislamu na kitaifa. Amesema, tayari kuna wasanii wengi ambao wamejiandaa vilivyo kutekeleza nara hiyo muhimu. Safarharandi ameutathmini mwaka uliopita wa Kiirani kuwa mwaka muhimu wa kunawiri masuala ya kiutamaduni na kisanaa nchini na kusema kuwa, uzoefu uliopatika katika uwanja huo unapasa kutumiwa kwa lengo la kufanikisha nara iliyotajwa ya marekebisho ya mwenendo wa matumizi nchini.
Amesisitiza kwamba, watu wanapasa kuchunguza masuala yanayopelekea kufanyika israfu katika maeneo yao ya kazi na nyumbani na hatimaye kuchukua hatua madhubuti za kurekebisha hali hiyo. 383040