Sabrina Troje ambaye anasomea shahada ya udaktari katika kitengo cha Paul Sabatier amenyimwa posho ya uhakiki kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya kukabidhiwa barua kutoka kwa kiongozi mpya wa chuo hicho akimtahadharisha juu ya uwezekanano wa kufukuzwa chuoni hapo kutokana na vazi lake la hijabu ya Kiisalmu.
Mfaransa huyo ambaye alichagua vazi la hijabu mwaka 2006, amekuwa akipokea posho ya kukamilisha utafiti wake wa shahada ya udaktari kila mwezi na anatazamiwa kufikishwa mahakamani kwa kukiuka sheria za idara za serikali.
Wakili wa Sabrina amesema ana matumaini kwamba mteja wake hatapatikana na hatia ya kukiuka sheria za idara za serikali kwa msaada wa taasisi zisizokuwa za serikali na jumuiya za kutetea haki za binadamu. 389985