Qasim Akademir amepewa nishani hiyo ya fahari kutokana na juhudi zake kubwa za kuimarisha mazungumzo kati ya dini mbalimbali na kuitisha mikutano na makongamano ya mara kwa mara.
Meya wa mji wa Donter nchini Uholanzi ambaye alihudhuria sherehe hizo amesema kuwa Akademir amefanya juhudi kubwa kama raia Muislamu wa Uholanzi za kuwaingiza Waislamu wenzake katika jamii ya nchi hiyo na kwamba maelewano yaliyopo kati ya wafuasi wa dini mbalimbali nchini Uholanzi yanatokana na jitihada kubwa za shakhsia huyo wa Kiislamu.
Meya wa mji wa Donter amesema anamkabidhi Akademir Nishani ya Fahari ya Ufalme wa Uholanzi kwa niaba ya malikia wa nchi hiyo. 398642