IQNA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran:

Harakati za Wazayuni kandokando ya msikiti wa al Aqsa ni kinyume cha sheri za kimataifa

17:22 - May 05, 2009
Habari ID: 1774117
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa harakati zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel za kupanua vituo vya Kiyahudi kandokando ya msikiti wa al Aqsa ni kinyume cha sheria za kimataifa na zinapingwa na wafuasi wa dini zote wakiwemo viongozi wa kidini wa kanisa la Orthodox huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Hassan Qaqshqavi amesema kuwa inasikitisha kuona kwamba mwenendo wa kupanua vituo vya Kiyahudi kandokando ya msikiti huo mtukufu umeshika kasi na kwamba suala hilo linapingwa na Waislamu wote na viongozi wa Kikristo hususan kanisa la Orthodox.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa jambo hilo linakiuka makubaliano yote ya kimataifa na sheria za mashirika yanayoshughulikia masuala ya utamaduni kama shirika la UNESCO. Qashqavi ameongeza kuwa hata wasiokuwa Waislamu wanaheshimu turathi za kidini na kusisitiza juu ya kulindwa maeneo hayo. Amesema kuwa jumuiya za dini mbalimbali zinasisitiza kuwa upanuzi wa vituo vya Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina haupaswi kufanyika sambamba na kuharibiwa turathi za kiutamaduni za dini nyingine.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelitaka Shirika la UNESCO, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na taasisi zote zinazoheshimu maeneo ya kiutamaduni kupinga vikali harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel za kupanua vituo vya Mayahudi kandokando ya msikiti mkongwe wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 399403
captcha