IQNA

Mfumo wa kisiasa Lebanon umegawa madaraka kati ya Waislamu na Wakristo

23:30 - May 10, 2009
Habari ID: 1776595
Mfumo wa Kisiasa Lebanon ni mfumo wa kikaumu ambao umegawa madaraka miongoni mwa Waislamu na Wakristo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, hayo yamesemwa na Mohammad Mutdhar Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Lebanon katika mkutano wake na wasomi kutoka Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Imam Khomeini (SA) ya Qum Iran na kuongeza kuwa, ‘bunge la Lebanon lina wajumbe 128 ambapo nusu yao ni Waislamu na nusu nyingine Wakristo’.
Ameendelea kusema kuwa, viti vya bunge vya Waislamu vinashikiliwa na Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Shia, Alawi na Druze na miongoni mwa Wakristo pia viti vimesambaa miongoni mwa makundi yote ya Kikristo nchini humo. 402722
captcha