IQNA

Muswada wa kupiga marufuku hijabu kuwasilishwa bungeni Marekani

19:04 - July 18, 2009
Habari ID: 1803520
Muswada wa sheria ya kupiga marufuku vazi la stara la mwanamke wa Kiislamu hijabu unatazamiwa kuanza kuchunguzwa hivi karibuni katika bunge la Oregon nchini Marekani.
Muswada huo iwapo itapitishwa na kuwa sheria utawapiga marufuku wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu katika sule za serikali na za umma.
Msemaji wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) Ibrahim Hoper amesema kuwa iwapo muswada huo utapasishwa na kuwa sheria utawalazimisha Waislamu kuchaguzia ama itikadi za dini yao au shughuli na kazi yao, suala ambalo amesema linatia wasiwasi mkubwa.
Ibrahim Hoper amesema kuwa kuvaa hijabu hakuna maana ya kuhubiri dini ya Kiislamu na kwamba katiba ya Marekani inatoa uhuru wa kutekeleza ibada kwa wafuasi wa dini mbalimbali.
Msemaji wa jumuiya ya CAIR amesema kuwa kupasishwa kwa muswada huo kutapingana na hotuba iliyotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani mjini Cairo Misri ambaye alisisitiza juu ya uhuru wa dini nchini Marekani. 435199
captcha