Taarifa ya Ekmeleddin Ihsanoglu imelipongeza Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa kulaani ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na ikasema: "Azimio la baraza hilo linasisitiza kuwa kuendelezwa ujenzi wa vitongoji hivyo kunakiuka haki za binadamu na maazimio ya Umoja wa Mataifa. Azimio hilo pia limesema, ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni huko Palestina unadhoofisha juhudi za kimataifa zinazofanywa kuhuisha mweneno wa amani Mashariki ya Kati.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lililokutana katika kikao chake cha 13 mjini Geneva vilevile limetoa limeutaka utawala ghasibu wa Israel kuwalipa Wapalestina fidia ya hasara zilizosababishwa na mashambulizi ya siku 22 ya utawala huo dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza. 555504