IQNA

Abdul Aziz Hakim, mmoja wa waanzilishi wa umoja wa Shia na Suni nchini Iraq

12:35 - August 15, 2010
Habari ID: 1973643
Sayyid Sadr Deen al-Qubanchi, Imam wa swala ya Ujumaa ya mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq amesema kuwa marehemu Sayyid Abdul Aziz Hakim, kiongozi wa zamani wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq alikuwa mmoja wa waanzilishi na washajiishaji wakuu wa umoja wa Kiislamu miongoni mwa Washia na Wasuni wa nchi hiyo.
Akizungumza hivi karibuni katika Swala ya Ijumaa ya mji huo kwa mnasaba wa kuwadia makumbusho ya kifo cha mwanazuoni huyo muhimu wa Kiislamu, al-Qubanchi amesema kuwa hatua ya Abdul Aziz ya kuanzisha Muungano wa Iraq Moja, ilikuwa hatua muhimu katika kuimarisha umoja, udugu, mapenzi na mshikamano wa Kiislamu miongoni mwa Washia na Wasuni na pia Waarabu na Wakurdi wa nchi hiyo. Ameendelea kusema kuwa marehemu Hakim alikuwa mwanafunzi aliyependwa na kuaminiwa sana na mwalimu wake Ayatullahil Udhma Shahid Muhammad Baqir Sadr na kwamba kwa muda wa karibu robo karne alikuwa msiri wa ndugu yake marehemu Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir Hakim, na wakati huohuo alitekeleza majukumu makubwa ya kijihadi na kisiasa.
Imam huyo wa Swala ya Ijumaa ya Najaf amemsifu marehemu Hakim kuwa mtu aliyekuwa na subira na kufanya juhudi kubwa kwa shabaha ya kuwaunganisha Waislamu.
Marehemu Hakim aliaga dunia tarehe 26 Agosti mwaka uliopita akiwa na umri wa miaka 59. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake hiyo al-Qubanchi amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kupinga kuhojiwa jeshi lake na Umoja wa Mataifa kuhusiana na hujuma liliyofanya dhidi ya msafara wa kimataifa wa misaada kwa watu wa Gaza. 632705
captcha