IQNA

Kongamano la Sita la Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu kufanyika mwezi ujao

15:26 - August 15, 2010
Habari ID: 1973911
Kongamano la Sita la Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu linatazamiwa kufanyika katika siku za tarehe 28 na 29 Agosti mwaka huu katika makao ya Jumuiya ya Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu mjini Tehran.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa kongamano hilo litafanyika kwa kaulimbiu ya 'Umoja, Mapambano na Ulimwengu Usiokuwa na Uzayuni' na kuhudhuriwa na wakurugenzi wakuu wa jumuiya za wanachuo wa nchi za Kiislamu.
Ajenda kuu ya kongamano hilo itatangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika Jumanne ya wiki hii. 633809


captcha