Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Nick Clegg amewapongeza kutokana na amali zao njema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hasa misaada ya kufuatia maafa ya mafuriko Pakistan na kusema: “Katika kusaidiana, Waislamu ni mfano wa kuigwa na watu wote duniani”.
Akizungmza Jumatatu usiku mjini London, Clegg amesema, ‘napongeza Shirika la Misaada la Kiislamu (Islamic Relief) kwa wito wake ambao umepelekea kukusanywa misaada ya dharura kwa waliokumbwa na maafa ya mafuriko nchini Pakistan”.
Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza amesema serikali ya London inaunga mkono Shirika la Misaada la Kiislamu na ametoa wito kwa wengine kuiga mfano wa shirika hilo.
Shirika la Misaada la Kiislamu ni taasisi ya kimataifa ambayo lengo lake ni kuwasaidia watu wa tabaka la chini zaidi duniani. Shirika hilo lilibuniwa nchini Uingereza mwaka 1984 na Dr. Hany el Banna nchini.
636460