IQNA

Askofu Mkuu wa Milan atoa wito wa kujengwa msikiti wa Waislamu katika mji huo

17:58 - September 06, 2010
Habari ID: 1989015
Askofu Mkuu wa mji wa Milan nchini Italia Kadinali Dionigi Tettamanzi amesema kuwa ni haki ya Waislamu kujenga maeneo ya ibada ya Kiislamu.
Gazeti la Zaman la Uturuki limeandika kuwa kufuatia matatizo yanayowakumba Waislamu wa mji wa Milan katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kutekeleza swala za jamaa, makundi ya Kiislamu yamewataka viongozi wa mji huo kuruhusu ujenzi wa msikiti mkubwa zaidi, ombi ambalo limekaribishwa pia na Askofu Mkuu wa Milan.
Kadinali Dionigi Tettamanzi amewaunga mkono Waislamu na akaongeza kuwa kwa mujibu wa sheria za Italia, Waislamu ambao ni wafuasi wa dini ya Mwenyezi Mungu, wana haki ya kuwa na maeneo ya ibada na kama wana tatizo kuhusu suala hilo linapaswa kutatuliwa haraka iwezekanavyo.
Hata hivyo wito huo wa Askofu Mkuu wa Milan limepingwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Roberto Maroni ambaye amekuwa akisikika mno kwenye vyombo vya habari kwa kutoa matamshi yanayopinga dini na wahamiaji nchini humo.
Awali makundi yenye misimamo mikali na yanayopiga vita Uislamu nchini Italia yalimshambulia Askofu Mkuu wa Milan Kadinali Dionigi Tettamanzi kwa kile wanachodai ni siasa zake za kulegeza kamba na kuwa na misimamo laini mbele ya Waislamu. 649449
captcha