Mashindano hayo yanasimamiwa na Idara ya Vijana na Michezo ya Kuwait kwa ushirikiano wa Idara ya Qur’ani ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo. Mashindano hayo yanafanyika katika sehemu mbili za wanawake na wanaume.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Vijana na Michezo ya Kuwait Jasim Yaqub amesema kuwa hadi sasa vikao kadhaa vimefanyika kati ya idara hiyo na Idara ya Masuala ya Qur’ani ya Wizara ya Wakfu kwa shabaha ya kuchunguza ratiba kamili ya mashindano hayo.
Amesisitiza kuwa mashindano hayo yana taathira kubwa katika kujenga shakhsia za vijana hao kwa mujibu wa mafundisho na thamani za Kiislamu na Qur’ani na ni hatua kubwa katika kuhudumia Qur’ani Tukufu na kueneza utamaduni wa kitabu hicho katika jamii hususan katika tabaka la vijana. 657754