Kwa mujibu wa shirika la habari la Malaysia 'Bernama' Mahathir Muhammad ameyasema hayo katika sherehe za kutunukiwa shahada ya fahari ya udaktari katika Chuo Kikuu cha USIM na kusisitiza kwamba ili kuweza kukabiliana na fikra zisizokuwa sahihi za Kimagharibi ambazo zinadhibiti fikra za walimwengu, maulama wa Kiislamu wanalazimika kutumia njia na mbinu za kisasa katika kulingania fikra za Kiislamu.
Ameongeza kuwa dunia ya sasa inakabiliwa na migogoro ya kimaadili, kijamii, kisiasa na kiuchumi kutokana na kudhibitiwa na itikadi na mitazamo ya Kimagharibi ambayo imebuniwa na wanafikra wa Magharibi bila ya kuzingatia msingi wowote wa kidini.
Mahathir Muhammad amesema kuwa fikra na mitazamo ya Kigharibi imebuniwa kwa njia ambayo inapotekelezwa katika jamii za Kiislamu hupelekea kupotoka jamii katika njia na malengo yake ya Kiislamu; kwa sababu hiyo wanafikra na maulama wa Kiislamu wanawajibika kutafuta njia na mbinu mpya za kukabiliana na fikra za Kimagharibi na migogoro ya kimataifa. 662793