Gazeti la al Shuruq linalochapishwa nchini Misri limeripori kuwa Jumuiya ya Waislamau wa Italia imepinga ubaguzi unaofanywa na wanachama na wafuasi wa chama cha mrengo wa kulia dhidi ya Waislamu huko kaskazini mwa nchi hiyo na kumwambia Rais Giorgio Napolitano wa nchi hiyo kwamba: "Kama rais wa nchi unapaswa kudhamini utekelezaji wa sheria, lakini kwa sasa uhuru wa kidini na heshima ya kibinadamu ya Waislamu wa kaskazini mwa nchi inayosisitizwa katika sheria na kanuni zote za Italia inapuuza na kukanyagwa."
Jumuiya ya Waislamu wa Italia imeashiria matamshi ya kichochezi ya baadhi ya viongozi wa kieneo na kusisitiza kuwa Waislamu wa kaskazini mwa nchi hiyo wananyimwa haki za kutekeleza kwa uhuru ibada zao za kidini na kwamba wamenyimwa hata haki ya kujenga maeneo ya ibada. 662240