Katika taarifa hiyo Prf. Ekmeleddin Ihsanoglu amewapongeza Waislamu kwa mnsaba wa Idul Adh'ha na kusema kuwa sikukuu hiyo ni rehma ya Mwenyezi Mungu na kutokea kwake siku moja baada ya Arafa na kukusanyika mamilioni ya Waislamu katika mlima wa Arafat kunakumbusha umoja na mshikamano wa umma wa Kiislamu na udharura wa kujiepusha na migawanyiko.
Katibu Mkuu wa OIC amesema hii leo Waislamu wanahitajia umoja na mshikamano kuliko wakati wowote mwingine kwa ajili ya kuzima njama zinazopangwa na maadui wao.
Ameongeza kuwa Waislamu wanahitajia umoja kwa ajili ya kulinda matukufu yao hususan kutetea Quds Tukufu mbele ya njama za utawala wa Kizayuni za kutaka kuuyahudisha mji huo na kuharibu utambulisho wake wa kiutamaduni na kihistoria.
Vilevile amewahimiza Waislamu kutowasahau wananchi walioathiriwa na mafuriko wa Pakistan. Amezishukuru nchi zote zilizotoa misaada kwa wananchi wa Pakistan na kuzitaka taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali kutoa misada zaidi kwa waathirika wa mafuriko hayo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu pia ametoa pendekezo la kuanzishwa taasisi ya kushughulikia hali ya Waislamu wakati wa maafa ya kimaumbile. 695844