Kituo cha upashaji habari cha Wizara ya Hija ya Saudi Arabia (Haj Information) kimeripoti kuwa zaidi ya waandishi habari 300 wa vyombo vya habari kote duniani ikiwa ni pamoja na kanali za televisheni za satalaiti na mashirika ya habari ya kimataifa yanaripoti habari za hija chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni na Habari ya Saudi Arabia.
Kwa sasa ofisi za Wizara ya Habari ya Saudi Arabia katika maeneo ya Jiddah, Makka, Madina, Arafat na Mina zimejaa waandishi habari wanaowakilisha vyombo vya habari vya kimataifa ambao wanafuatilia na kuripoti amali za ibada ya hija katika maeneo matakatifu hadi mwishoni mwa ibada hiyo.
Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu mapema leo walielekea Mina ambako wanafanya ibada za kumpiga mawe shetani, kukata nywele na kuchinja mnyama wa sadaka kabla ya kuelekea katika msikiti mtakatifu wa Makka kwa ajili ya twawafu. 696685