Hujjatul Islam Walmuslimin al Qubanchi amesema kuwa Idi ya Ghadir Khum ina nukta mbili muhimu ambazo kwanza ni kubainisha kuwa mawasiliano baina ya mbinu na ardhi hayakukatika baada ya kuaga dunia Mtume Muhammad (saw), na pili ni kuwa mawasiliano hayo yataendelea hadi siku ya Kiyama kupitia huja wa Mwenyezi Mungu.
Imam wa Sala ya Ijumaa ya Najaf amebainisha tukio la Ghadir Khum kwa kutegemea aya za Qur'ani Tukufu na kusema kuwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kujenga uhusiano naye na kujisalimisha kwake humpa mwanadamu utulivu wa kiroho.
Vilevile amewataka viongozi wa serikali ya Iraq kuteuwa watu wanaostahiki, wenye ikhlasi na wasafi katika nyadhifa mbalimbali za serikali. 697873