Kituo cha habari cha Haj Information kimeripoti kuwa wafanyakazi hao zaidi ya elfu tano watatumia mashine 300 kutekeleza mpango wa Halmashauri ya Jiji la Makka wa kusafisha mji huo baada ya kumalizika shughuli za hija.
Mpango huo unajumuisha maeneo ya Mina, Arafat na Muzdalifa.
Hamlashauri ya jiji la Makka pia itatumia ndege za Wizara ya Kilimo ya Saudi Arabia kunyunyizia dawa katika maeneo matakatifu ya Makka.
Karibu mahujaji milioni tatu kutoka maeneo mbalimbali duniani wametekeleza ibada ya hija mwaka huu huko Saudi Arabia. 699959