Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanachuo waliotembelea nyumba hiyo wamefafanuliwa kuhusu maisha ya mapambano ya hayati Imam Khomeini tangu alipoanza harakati za mapambano hadi ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, matukio ya baada ya mapinduzi hadi alipoaga dunia.
Wanachuo wa kigeni wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) vile vile walitembelea eneo la kutengenezea Zarih ya Haram ya Imam Hussein AS.
Itakumbukwa kuwa olimpiadi ya wanaume ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW ilimalizika Novemba 21 katika mji wa Qum nchini Iran. Olimpiadi ya wanawake iliendelea hadi Novemba 22.
Sherehe za kuwatunukia zawadi washindi Olimpiadi ya 16 ya Qur'ani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) zitafanyika Jumatano tarehe 24 Novemba.
700053