IQNA

Walimu wenye vazi la hijabu wazuiwa kufundisha Uholanzi

7:32 - November 30, 2010
Habari ID: 2039889
Shule moja ya msingi inayomilikiwa na Wakristo Waorthodox katika mji wa The Hague nchini Uholanzi imekataa kumuajiri mwalimu Muislamu kwa sababu ya kuvaa vazi la stara la mwanamke wa Kiislamu, Hijabu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Dutch News, Teun Klaver Mkuu wa shule husika amedai kuwa mavazi ya Kiislamu ni marufuku shuleni hapo. Amesema kuwa mavazi ya Kikristo ndio tu yanayoruhusiwa katika shule hiyo.
Msemaji wa Tume ya Fursa Sawa nchini Uholanzi amesema: 'Shule hiyo ni ya Wakristo Waorthodox wa Uholanzi na inaendeshwa kwa njia binafsi lakini hupokea bajeti ya serikali na inaruhisiwa tu kuzuia nembo za kidini iwapo kuna dharura'.
Kumekuwepo na ongezeko kubwa za chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya na hasa Uholanzi na ni katika fremu hiyo ndio maana wanawake Waislamu wanabaguliwa na kuzuiwa kuvaa vazi la Hijabu.
703960

captcha