Mwakilishi asiyekuwa Mwislamu wa chama cha Uadilifu nchini Malaysia ametumia aya za Qur'ani Tukufu kutia nguvu hoja zake katika mkutano wa kila mwaka wa chama hicho, suala ambalo limewavutia Waislamu wengi nchini humo.
Gavana wa jimbo la Salangor nchinio Malaysia Abdul Khalid Ibrahim amesema kuwa hatua ya mwakilishi Kisawan ya kunukuu aya za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika mkutano wa kila mwaka wa chama cha Uadilifu ni ishara ya nafasi ya juu ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu katika jamii ya nchi hiyo na mafanikio yanayopaswa kutiliwa maanani, kwani hatua hiyo inawafundisha watu wengine kutegemea maandishi ya kitabu hicho katika mambo mbalimbali.
Gavana Abdul Khalid amesema, mwakilishi asiyemwislamu wa chama cha Uadilifu amesema kuwa Qur'ani inawalazimisha watu wote kutekeleza vyema majukumu na wajibu wao.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa chama cha Uadilifu cha Malaysia ni chama chenye mielekeo ya wastani ambacho kiliasisiwa mwaka 2003.