IQNA

Mkutano wa kimataifa wa bidhaa Halal wafanyika Pakistan

15:27 - December 05, 2010
Habari ID: 2042139
Kongamano la Kimataifa la Halal limefanyika Disemba nne huko Karachi nchini Pakistan na kuwakutanisha pamoja wasomi na wataalamu 25 maarufu kutoka nchi 17 duniani.
Kongamano la Kimataifa la Halal limeandaliwa na Halmashauri ya Biashara na Maendeleo Pakistan kwa ushirikiano wa Baraza la Ustawi wa Bidhaa Halali.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kusisitiza umuhimu wa bidhaa halali na kueneza ufahamu wa umuhimu wa bidhaa halali hasa katika nchi zisizo za Kiislamu.
Akizungumza katika kongamano hilo Spika wa Bunge la Pakistan Dr. Fehmida Mirza amesema bunge hilo litapitisha sheria ya kuhimiza uuzaji na usambazwaji bidhaa halali. Mufti wa Bosnia Herzegovina Dr. Mustufa Ceric pia amehudhuria kikao hicho na kutoa wito kwa nchi za Kiislamu kuzingatia viwango, ladha na ubora wa bidhaa wakati wa kuuza vyakula halali duniani.
706222
captcha