IQNA

Waziri wa Ujerumani kukutana na wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu

17:15 - December 05, 2010
Habari ID: 2042686
Thomas de Maiziere Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani amepanga kukutana na kubadilishana mawazo na wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu za nchi hiyo mjini Bonn hapo siku ya Jumatano tarehe 8 Disemba.
Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa waziri huyo atakutana na maimamu wa misikiti na wawakilishi wa jumuiya kadhaa za Kiislamu za Ujerumani ili kujadili suala la kupewa mafunzo maalumu wafanyakazi wa taasisi za kidini na wasimamizi wa misikiti na vituo vya Kiislamu vya nchi hiyo.
Njia za kuandaa uwanja wa kuimarishwa mfungamano wa watu na misikiti, mafunzo kwa maimamu wa swala za jamaa, masomo ya lugha ya Kijerumani kwa wafanyakazi wa misikiti na taasisi za kidini na Kiislamu na pia kupitishwa mpango wa masomo katika Muungano wa Kiislamu wa Ujerumani ni baadhi ya masuala muhimu yatakayojadiliwa katika mazungumzo hayo.
Ujerumani ina zaidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu 2600 ambapo maimamu wa swala za jamaa na wanazuoni 2000 wanajishughulisha na masuala tofauti katika vituo hivyo vya kidini. 705943
captcha