Serikali ya nchi hiyo imewaamuru askari usalama kukusanya vitambaa na mabango yaliyoandikwa maandishi ya maombolezo ya Imam Hussein (as) na vilevile kuweka askari wazuia-ghasia katika njia wanazopitia waombolezaji pamoja na Husseiniya za baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
Taarifa hiyo imebainisha masikitiko ya wanazuoni wa Kishia ambao wamesema kuwa walitaraji serikali kuchua hatua zinazofaa na za kimantiki kwa ajili ya kutayarisha mazingira mazuri ya Waislamu wa Barain kuishi pamoja kwa amani na utulivu na hasa katika mwezi huu mtukufu wa Muharram lakini kwamba kitendo cha hivi karibuni cha serikali hiyo dhidi ya Mashia kinaashiria kinyume cha matarajio hayo.
Wamesema kitendo cha polisi na askari usalama hakionyeshi jambo jingine isipokuwa dharau ya wazi dhidi ya matukufu ya Imam Hussein (as) wafuasi wa Ahlul Beit (as) na thamani za kidini dhidi ya madhehebu maalumu. Wamesema kitendo hicho bila shaka kimelenga kuvuruga utulivu uliopo kati ya madhehebu za Kiislamu za nchi hiyo.
Baraza hilo la maulama wa Kishia limetaka kusimamishwa kitendo hicho cha dharau mara moja katika pembe zote za nchi na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Limesema dharau hiyo kamwe hautapunguza utiifu na imani ya Mashia wa nchi hiyo kwa Ahlul Beit (as) bali itaimarisha zaidi imani hiyo ya kidini. 710181