IQNA

Mwalimu Shia afukuzwa kazi kwa sababu ya kufundisha swala!

14:23 - December 22, 2010
Habari ID: 2051775
Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia imemfukuza kazi mwalimu mmoja mfuasi wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia kwa sababu tu ya kufunza wanafunzi ibada ya swala kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul Bait (sa) na kutoa zawadi ya vitabu vya kidini kwa wanafunzi wake.
Kanali ya habari ya Rasid imeripoti kuwa maafisa wa Wizara ya Elimu ya Saudia wamemtimua kazi Fauzi Shanar ambaye ni mwalimu katika mkoa wa Qatif kwa tuhuma za kufunza swala kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlulbaiti wa Mtume (saw) na kutoa zawadi ya vitabu vya kidini kwa wanafunzi wake.
Tuhuma hizo zilitolewa dhidi ya Fauzi Shanar mwaka uliopita wa masomo na kesi hiyo iliendelea kwa miezi kadhaa hadi jana ambapo Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia ilitoa hukumu ya kumuachisha kazi rasmi mwalimu huyo.
Mwalimu huyo mfuasi wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia aliyekuwa akifundisha katika shule ya msingi ya Suhaib al Rumi katika mji wa Saihat mkoani Qatif, amewahi kujadiliana na walimu wenzake wa Kiwahabi katika shule hiyo.
Fauzi Shanar ni mwalimu na mwanaharakati wa Kishia ambaye ni maarufu katika eneo anakoishi kwa kuwa na uhusiano mzuri wa kijamii na wakazi wa eneo hilo. 716549
captcha